Waziri Mwakyembe Awatolea Povu Wasanii Wanaokosoa Tozo Ya Milioni 5 Kutoka BASATA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewatolea povu wasanii mbali mbali ambao wamekuwa wako Paz’s sauti na kukoso ada mpya zilizotolewa na BASATA.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa ada hiyo ya milioni 5 haiwahusu kabisa wasanii kwani inatozwa kwa makampuni lakini anashangaa wasanii wamekuwa mstari wa mbele kukataa tozo hiyo kuliko hata makampuni yenyewe.

download latest music    

Wasanii wengi kama Nikki wa Pili, Bill Nas na wengineo walikosoa tozo hiyo kubwa na kudai itapelekea makampuni kupunguza matangazo na wasanii, Mwakyembe amesema kuwa hakuna kampuni isiyotaka faida hivyo kamwe makampuni hayawezi kuacha kuwatumia wasanii.

Lakini baada ya mkutano wa muda mrefu kuhusu kubadilisha tozo hiyo Waziri Mwakyembe aliwataka wasanii wachache pamoja na wadau wa sanaa wakae na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kujadili namna kubadili huo mfumo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.