Wema Afungiwa Miaka Miwili Kutofanya Sanaa.

Chama cha filamu  Kinondoni  TFDAA kimemfungia kufanya kazi  zozote za filamu mwana dada Wema Sepetu kwa muda wa miaka miwili kuanzia tamko jilo kutolewa mpaka litakapotimia miaka miwili ijayo.Adhabu hiyo ni muendelezo wa adhabu zinazoendelea kutolewa na mamlaka mbalimbali kumlenga wema baada ya kusambaza video zinazoenda kinyume na maadili ya jamii.

Chama icho kimeenda mbali zaidi na kusema kuwa kwa muda huu  vyama vingine havipaswi kumsikiliza msanii huyo akiwa anakuomba misamaha na kupuuza misamaha anayoomba .Msemaji wa kamati ya chama icho anasema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kamati ya maadili kukaa chini na kufikia muafaka huo.

download latest music    

Chama icho kinasema kuwa ni matumaini yao kuwa BASATA pia watamuongezea adhab mwanadada huyo kutofanya kazi kwa muda ili kuonyesha kujifunza kwake mwa muda wa miaka miwili ili aweze kujirekebisha.

Mpaka sasa BASATA wamepeleka kesi mahakamani kwa ajili ya kushughulikia kesi hiyo inayomkabili Wema sepetu  ya utovu wa nidhamu na uchapishaji video zenye maudhui ya kingono.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.