Loading...

Wema Afungukia Kurudi CCM, Asema Mambo ni Magumu

December 07, 2017 at 07:26
Wema Afungukia Kurudi CCM, Asema Mambo ni Magumu

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu msanii Wema Sepetu kurudi CCM akitokea CHADEMA  na kukaa kimya kwa muda , mwanadada huyo ameamua kufunguka na kusema yale anayoyaona na kuyafikiria baada ya kufanya uamuzi huo.Pamoja na kwamba ameamua kusema kile anachokutana nacho lakini msanii huyo anasema kuwa hawezi kuzungumza sana mambo hayo kwa sababu bado anaweka vitu sawa lakini kuna mambo mengi yanayomfanya akate tamaa kwa sasa.

Its too copmlicated najikuta sipo kwenye position ya kuelezea in simple english au kiswahili  siwezi ila tubaki tu tunamuomba Mwenyezi Mungu  kwamba everything will be fine one day, Inshallah.

I am strong, kama nisinge kuwa strong wala sasa hivi nisingekuwa hapa kweli,najaribu kusali kwa hii hali muda mwingi kama binadamu inaweza kukuvunja moyo na kukufanya ukate tamaa.Yaaan its ok ngoja nimuachie Mungu

Wema sepetu alikuwa CCM kwa mara ya kwanza na baadae alikuja akahamia CHADEMA na mama yake mzazi ambapo amekaa kwa muda kama miezi sita na kuamua kurudi tena CCM ambapo yeye anakuhita nyumbani na kwamba kule alipokuwa hakuwa na amani, ingawa mama yake amekanusha na kukataa kurudi CCM.

Loading...

Akiwa kama msanii Wema anaejulikana na kupendwa na watu , baada ya kujiingiza katika wimbi hilo la siasa amejikuta akisemwa sana katika mitandoa na baadhi ya mashabiki ambao wanaamini ku wa kitendo cha yeye kuhama hama kisiasa pia kuna haribu na kupoteza umakini wake katika kazi zake na kuwafanya mashabiki zake pia kutokuwa na muelekeo mzuri, hata hivyo Wema amekuwa akikukutana na changamoto nyingi zinazomfanya mpaka kukata tamaa.

kwa siku za karibuni wema sepetu amekuwa akionekana ni mtu wa kukata tamaa na kufikia hatua ya kutamani kufa kutokana na yale anayokutana nayo yanayofanya maisha yake yanakuwa magumu na kushindwa kuishi kwa amani.

Hata hivyo ugumu wa maisha ya siasa kwa wema unakua pale baada ya kutangaza kurudi , vyama vyote vilionekana kupuuzia matamko yake huku baadhi ya viongozi wa Chadema wakisema kuwa alipoamia kule hakuwa mwanachama halisi bali akuwa mfuasi tu kama watu wengine huku CCM wakimwambia kuwa inabidi aanze upya kuomba uanachama sio kuhama na kurudi pale anapojisikia,

 

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.