Wema Aita Waandishi wa Habari, Aomba Radhi Mashabiki na Serikali.

Mwanadada Wema sepetu amewaita waaandishi wa habari mapema leo nyumbani kwake na kuongea nao huku dhumuni lake kubwa ikiwa ni kuataka kuombamsahama kwa mamalka husika na mashabiki zake wote kutokana na video chafu iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa faragha na mume wake mtarajiwa.

Wema anasema kuwa amekiri kosa hilo na hawezi kutaja sababu ya kwanini alifanya hivyo zaidi ya kujutia kosa hilo kwa sababu amedahlilisha watu wengi na kuwaumiza hasa wale wanaompenda ikiwepo mama yake mzazi.

download latest music    

Naomba radhi kwa hili liliotokea, naomba radhi kwanza kabisa kwa serikali yangu kupitia mamlaka ya TCRA , naomba radhi kwa bodi yangu ya filamu na pia naomba radhi kwa familiayangu, ndugu jamaa na marafiki, naomba radhi kwa wale wote wanaonipenda .

nawaomba radhi wadogo zangu ambao wamekuwa wakiniangalia kama kioo kwao, lakini zaidi namuomba radhi mama yangu mzazi , najua nimewadharirisha wengi na wala siko hapa kutoa sababu ya kile nilichokifanya  kwa sababu haitabadilisha kile kilichotokea lakini pia sihitaji kumlaumu mtu yoyote kwa lililotendeka kwa maana kosa ni kosa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.