Wema Atangaza Ujio Wa Lipstick Zake Baada Ya Kufungiwa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Wema Sepetu amerudi kwa kasi ya ajabu katika ulimwengu wa Biashara ya lipstick baada ya kufungiwa kwa muda na biashara kusimama.

Wema alikuja na bidhaa hizo kwa mara ya kwanza miaka michache iliyopita lakini baadae zilikuja kufungiwa na TFDA kwa kukosa vigezo vya Kutumia na binadamu.

download latest music    

Wema amerudi Tena bidhaa hizo ambapo atakutana na mashabiki wake pamoja na wakazi wote wa Arusha kwa siku mbili mfululizo kuwauzia bidhaa zake mpya za Lipsticks ambazo mashabiki wake walizimiss kwa miaka miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema amesema kuwa ataanza kuuza bidhaa hizo mkoani Arusha kwa siku mbili kuanza tarehe 26 hadi 27 Aprili 2018, ambapo yeye mwenyewe ndiye atakayekuwa anahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma, katika duka la Kubrasadiki.

Good News For you, Tunakuja week hii tar 26 na 27… Tutakuwepo kwenye Duka la Wakala wetu Mkubwa wa Arusha @kubrasadiki @kubrasadiki @kubrasadiki. Na nitakuuzia Lipstick mwenyewe… Cant wait kumeet warembo wangu…. Alhamis na Ijumaa hii Ladies & Gents”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.