Loading...

“Wema Bado Yupo Kifungoni”- Bodi Ya Filamu

January 11, 2019 at 07:54
“Wema Bado Yupo Kifungoni”- Bodi Ya Filamu

Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo amesema msanii wa filamu, Wema Sepetu hajafunguliwa kujihusisha na masuala ya uigizaji kama inavyovumishwa mitandaoni.

Bodi ya filamu Tanzania imetoa tamko hilo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Baada ya tetesi kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Wema amemaliza adhabu yake.

download latest music    

Karibu mtendaji amesema kuwa endapo msanii huyo atafunguliwa Baraza hilo litaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kulieleza jambo hilo na si kama inavyoelezwa kwenye mitandano ya kijamii.

Jamaninaombeni muachane na stori za mitandaoni, Wema bado yupo kifungoni na endapo itatokea akaruhusiwa kujihusisha na masuala ya uigizaji bodi itaitisha mkutano na wandishi wa habari na kila mtu atajua,”.

Wema Sepetu alipewa adhabu hiyo ya kufungiwa kujihusisha na kazi za sanaa mwaka jana Oktoba 26 baada ya kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment