Wema Kurudi CCM Wazee Walishaongea, Aliondoka Kwa Hasira Tu- Steve Nyerere

December 07, 2017 at 08:43
Wema Kurudi CCM Wazee Walishaongea, Aliondoka Kwa Hasira Tu- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie na mwanasiasa Steve Nyerere amezidi kufunguka tena kuhusiana na kitendo cha Wema Sepetu kurudi tena CCM baada ya kuhama Chadema na kudai kuwa Wema karudi CCM kwa sababu wazee walishaongea ili iwe hivyo.

Wikiend iliyopita muigizaji Wema Sepetu aliwashtua watu wengi baada ya kutangaza kuwa ana rudi rasmi katika chama chake cha siasaCCM huku akikiita ndio nyumba kwake. Jambo hilo liliwashtua watu wengi kwa sababu February 24 mwaka 2017 Wema alitangaza rasmi kuwa yeye na Mama yake mzazi wanahamia Chadema rasmi kutokana na kile walichodai ni mgongano wa itikadi kwaiyo December mosi mwaka huu alivyotangaza kuwa anarudi CCM alizidi kuwashangaza watu wengi.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Steve Nyerere amefunguka na kudai kuwa Wema kurudi CCM ni kitendo ambacho wazee walishakiongelea:

Hakuna asiyejua kuwa Wema alizunguka nchi nzima katika harakati za kumtafutia kura Raisi wetu na yeye kwa njia moja au nyingine ndiye amesababisha tulishinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu, Wema aliondoka CCM kwa hasira tu lakini ameona maisha magumu ameamua kurudi nyumbani basi tumpokee na tumkanye ili asirudie tena na hapa lazima tumpongeze Wema kwa kurudi nyumbani lakini tangu alipohama CCM kuna wazee waliyazungumza na walizungumza naye ila sisi wengine ni vichochezi tu”.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku za karibuni Wema amekiri kuwa kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana na kinachomsaidia ni maombi kwa Mungu lakini hajajutia uamuzi wake wa kurudi CCM.

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.