Wema Sepetu Aingilia Kati Ugomvi wa Zari na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu ameingilia kati na kutoa yake ya moyoni kuhusu kinachoendelea hivi sasa kati ya wapendanao Diamond na Zari.

Wiki iliyopita siku ya Valentine’s Day Zari alishangaza wengi baada ya kutangaza kumbwaga aliyekuwa mpenzi wake na baba watoto wake Diamond huku akidai sababu kubwa ni skendo na uchepukaji wake uliokithiri.

download latest music    

Tangu waachane Wema amekuwa akitajwa sana na watu mbali mbali huku tetesi zote zikidai kuwa Wema amerudi kwa Diamond jambo ambalo limekuwa likisemwa kwa muda mrefu tangu kabla hata Diamond hajaachana na Zari.

Wema amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na uhusiano wa Diamond na Zari na kuzungumzia hasa kinachoendelea hivi sasa baina yao ambapo kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online Wema alisema yafuatayo:

Kama kweli wameachana basi wayamalize tu na maisha yaendelee ingawa mapenzi hayaingiliwi warudiane ili walee watoto wao kwa pamoja”.

Lakini pia Kwenye interview hiyo aliyofanya na Dizzim Online Wema alifunguka kuhusiana na Account yake ya Instagram ambayo imeibiwa kwa wiki kadhaa sasa ambapo amesema kuwa anawaomba mashabiki zake kuwa na moyo wa subira kwani bado anaendelea  na jitihada za kuirudisha mikononi mwake.

 

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.