Wema Sepetu akesha akimlilia Tundu Lissu

Tukio la kushambuliwa na kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye ni wakili na Mwanasheria mkuu wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Limewaliza wengi ikiwemo staa wa Bongo movies, Wema Isaack Sepetu ambaye anadaiwa kukesha akilia hivyo kuibua sintofahamu kwa watu waliomzunguka kwa mujibu wa marafiki  wa karibu wa Wema wamesema kuwa taarifa hizo zilimchanganya hasa ukizingatia kuwa Lissu ni ndugu yake na pia ni waili wake katika kesi inayomkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya. Baada ya Wema kupata taarifa hizo aliangua kilio usiku na mchana kutwa, mwishoni mwa wiki iliyopita alibadilisha staili ambapo alikuwa halii badala yake aliamua kujifungia ndania akimuombea kiongozi huyo . Wema alipoulizwa kama madai hayo yana ukweli wowowte alijibu:

“Hakuna kitu kilichoniumiza kama  hicho na bado kitaendelea kuniumiza hadi nione anko Lissu anaendelea vizuri kama mwanzoni”.

download latest music    

Mheshimiwa Lissu anasemekana kuendelea vizuri tangu asafirishwe kupelekwa Nairobi, Kenya kwaajili ya matibabu zaidi. Wema alijenga ukaribu na Lissu baada ya kuhamia Chadema mapema mwaka huu baada ya kukabiliwa na kesi ya kuuza na kutumia madawa ya kulevya ambapo pia Lissu alikuwa mmoja kati ya mawakili wake pia katika ukurasa wake wa instagram Wema aliandika:

“…Nini hiki jamani…??? Oh lord help my Uncle… If anything happens to him then nadhani wengi wetu vitatutokea maana hatutokaa KIMYA..!! Ni kutokaa kimya ndo kumempelekea haya yote kutokea.. Nimeikumbuka Tanzania tetu ya miaka miwili iliyopita…sio Tanzania hii isiyo na amani ..Am praying for my Uncle Lissu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.