Wema Sepetu Atinga Bodi Ya Filamu Kuomba Kufutiwa Adhabu

Staa wa filamu za Bongo movie Wema Abraham Sepetu siku ya jana ametangaza katika Otis I ya bodi za filamu Tanzania kwa ajili ya kuomba kupunguziwa adhabu aliyopewa Baada skendo yake.

Wiki chache zilizopita Wema Sepetu alifungiwa kujihusisha na filamu katika kipindi kisichojulikana baada ya kuposti video zake za faragha za chumbani kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

Siku ya jana Wema aliwasili katika Ofisi za bodi ya filamu kwa lengo la kuangalia Kama anaweza kupunguziwa adhabu yake ambapo alijitetea kuwa amekuwa na mwenendo mzuri na kusema:

Filamu ndio kitu ninacho kitegemea kwenye maisha yangu na tangu nimefungiwa nimekosa fursa nyingi za kazi ambazo zingetutangaza kimataifa, hivyo naahidi kuendelea kuwa na mwenendo chanya katika jamii pasipo kuharibu maelekezo niliyopewa na Bodi ya Filamu katika kuisafisha taswira yangu ambayo imechafuka”.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo Alieleza kuridhishwa na mwenendo wa Wema Sepetu  kufuatia utiifu wake wa adhabu aliyopewa na kusema Tasnia ya Filamu bado inamuhitaji na kama akiendelea na mwenendo mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa.

Tunamuhitaji sana Wema Sepetu katika Tasnia ya Filamu kutokana na umahiri wake katika kazi lakini tunachukia maadili mabovu aliyoyaonesha katika jamii na sisi kama Bodi ya Filamu hatutasita kumfungia moja kwa moja kama akiendelea na matendo yauvunjifu wa maadili yetu kama Watanzania”.

Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Wema Sepetu kuhakikisha anarudisha Taswira yake chanya iliyopotea na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na ikiwa mwenendo wake utazidi kuwa mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.