Wema Sepetu: “Sijakatwa Utumbo, Nimekonda Kwa Mawazo”.

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu ameibuka na kuweka wazi kuwa yeye hajakonda Kwajili ya kukatwa utumbo kama inavyodaiwa bali amekonda kwa ajili ya mawazo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema kwa mara ya kwanza aliweka ‘plain’ kuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

download latest music    

Watu nawashangaa sana, wanaona kukatwa utumbo ni kitu rahisi ee? Mimi nimekon­da kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine maana nilikuwa kwenye wakati mgumu sana”.

Lakini pia Wema ameongeza kwa kusema kwamba, licha ya kupungua anaufurahia muonekano wake mpya kwani kuwa mnene zaidi nayo siyo poa.

Yaani hujui tu ninavyoufura­hia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka na napendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.