Loading…

Wolper Afunguka Mazito Juu ya Harmonize

September 12, 2017 at 18:56
Wolper Afunguka Mazito Juu ya Harmonize

Ni siku chache tangu msanii jackline wolper aamue kufunguka kuhusu sababu ya yeye kuachana na mpenzi wake wa zamani harmonize msanii kutoka katika lebel kubwa ya wcb, ikumbukwe kuwa wawili hao walikuwa katika mahusino ya kimapenzi na walionekana kuwa na mahaba mazito sana.lakini walikuja kuachana na wolper alipozungumza kuhusa sabau ya kuachana kwao alisema sababu ni mahusiano mapya ya msanii harmonize na mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina kwa jina la sarah. Leo imezuka tafrani nyingine katika mtandao wa instagram  baada ya  wolper kutoa majibu ya  wimbo mpya wa harmonize  uliojulikana kwa jina la ‘NISHACHOKA’ ambapo wimbo huo unadhaniwa kuwa ni kibao kilicholenga kumsasambua wolper. wimbo huo unaonyesha kusimulia maisha yao ya kimahusiano na kufichua baadhi ya mambo. Kuna baadhi ya mistari inasema   ‘kisicho riziki hakiliki….naandika huu wimbo usidhani kama nakufikiria..’

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram jackline wopler huku maneno hayo yakionesha yanania ya  kumjibu  maneno yaliyoyasemwa  kwenye wimbo huo.wolper ameonyesha kudharau kipaji cha harmonize kwa kumwambia kuwa sasa ameanza kuingia kwenye taarabu,na kwamba hata yeye akiamua kuimba hawezi kuimba kama yeye.

Loading...

Wolper amekuwa  amemshushua harmonize kwa maneno aliyoyaimba ambayo yanapinga na ukweli ‘Unanitungia nyimbo alafu unasema ooo unifikirii mtu mpk unaingia studio unaimba mipasho yako si inamaana nimekujaa kwenye koo mpk mwili yani mpk tukikupima group lako la damu tunaweza kupata WOLPER MASSAWE” aliandika wolper

Katika ujumbe huo wolper ameamua kufunguka mazito ambayo yalikuwa yanafanyika katika mahusiano yaoambapo  kwa namna moja ama nyingine hakuwahi kuyaongea kama chanzo cha mafarakano yao “Sikiliza nimelala chini,Nimekufumania,Nimekuta msgz za wanaokutafutia wanawake lkn sijawahi kuongea kwasababu najua nn maana ya mahusiano kuna kuachana ”  ameandika wolper

Hata hivyo wolper amemtaka mpenzi wake huyo wa zamani kuimba wimbo mpya ili azungumze na mengine mazuri aliyokuwa anamfanyia kama kumsubiri studio,kulia sana kwa ajili yake na ikibidi aimbe nyimbo za kumsifia mwanamke wake mpya anaejulikana kwa jina la Sarah.

 

Comments

  1. HARMONIZE ALIPOTEZA MTU WA MAANA,ATAFUNZWA NA DUNIA

  2. Maskini wolper mapenzi yanakuumiza sana, usijali na hawa watundu wa WCB wapuuzi sana

  3. WCB ideas zimeanza kuishi lazima wataje watu kupata kiki

  4. Mariam Abubakar : September 13, 2017 at 10:42 am

    Heri harmorapa sasa,huyu mkaka anapotea kwa kuiga kila bosi wake anachofanya,utaskia pia ana mtoto hivi karibn

  5. Hawa WCB wanaudhi sana, imbeni taarabu kama bongo flava imewashinda. Yaani kiba amewapasua vichwa mpaka ushenzi wao umefikia hapa,pole sana Wolper

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.