Wolper amrarua Madee kwa kutumia katuni yake

Jacqueline Wolper amekerwa na hatua ya Madee kutumia katuni ya picha yake bila idhini yake kwenye video ya wimbo wake ‘Sikila’ aliyomshirikisha msanii Tekno kutoko Nigeria.

Mrembo huyo alidhihirisha kuwa hakufurahia alichofanya Madee kwa mtandao wa Instagram ambapo aliweka picha ya katuni yake na kuiambatanisha na ujumbe mrefu:

download latest music    
Picha ya katuni ya Wolper aliyotumia Madee kwenye video yake

“Hebu ona jamani, macho yanatia huruma kama nina upwiro kilo 200. Hii mikaka yetu ya Kibongo kuna muda inaboa, kuna muda inakuwa poa. Sasa Madee, Rais wa Manzese nikuulize swali, ulishindwa nini kunyanyua ka simu kako na kunipigia hata kinafiki na kuniambia unani-video queen katuni, sijui sanamu?

“Unajua wewe, acha dharau, wewe pumbavu, piga simu, omba kwanza, hata kama humlipi mtu, sisi tunasaidiana, wote wasanii, leo kwangu, kesho kwako na kunishika kimahaba, umenishika, una dhambi wewe kaka na suti umenivalia kama unaenda kutoa posa kwa Masawe.

Madee

“Sasa onyo, siku nyingine omba utapewa, acha kuparamia kama vile unaomba raundi kwa kimada wako, kwanza unitafute utoe hata faini ya kuniweka macho kama nimevuta ugoro.

“Ila nyimbo kali, nisiwe mchoyo na nimependa idea ila mwambie alinichonga na kunipa hiyo shepu nitampasua,” Wolper aliandika.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere