Loading…

Wolper na Harmonize ndani ya Bifu Zito

September 12, 2017 at 19:25
Wolper na Harmonize ndani ya Bifu Zito

Mwigizaji wa Bongo movies Jackline Wolper na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize wamejikuta katika bifu zito baada ya kuingia katika vita ya kurushiana maneno mtandaoni.  Wolper na Harmonize waliachana miezi michache iliyopta kwa kile alichokidai Wolper kuwa Harmonize alimsaliti na kutembea na msichana mwingine anayejulikana kwa jina la Sarah, katika mahojiano aliyoyafanya Wolper hivi karibuni alielezea machungu aliyoyapata baada ya kugundua kuwa Harmonize anatembea na msichana huyo mwingine kwa ajili ya tamaa ya pesa.

Baada ya kukaa kimya bila kutoa maelezo yoyote siku ya leo Harmonize ameachia wimbo wake mpya unaojulikana kama “Nimechoka” wimbo aliomuimbia mpenzi wake wa zamani Wolper wimbo ambao alituma kwenye ukurasa wake wa instagram na ujumbe usomao:

Loading...

“Naomba nikupe jukumu la kumtumia #EX wako ambae kila kukicha anakuzumgumzia tena kwa ubaya na kutengenezea mazingira ya chuki katika jamii na umwambie nimechoka”, “Tena mwambie asijekuwa anajidanganya eti unamuwaza…!!! Ni kwasababu umeumbwa na stara hunaga uropo ropo wa kuongea vya ndani pia unaweza kung’oa mkali zaidi yake”.

Wolper naye kwa kupitia ukurasa wake pia alimjia juu Harmonize na kumrushia maneno:

“…Tusilazimishane kuongea nimeshaachana na wewe kiusalama ongelea vilivyopo kwako saivi sio mimi, Nilishatokaga huko kirahisi unaweza ukadeal na style yako ya mziki bila kunihusisha maana unampa hofu pia BFF anahisi labda kuna kitu kumbe hakuna, usiniharibie mahusiano yangu mapya , BFF wangu ni bora kuliko wewe ni adimu na sitaki kumpoteza kwa ajili ya watu kama wewe…Mimi ni Jackie Wolper ambae siwezi kuacha kuongea ukinianza namaliza kwa wale wanaosema bora kunyamaza subirini yawakute alafu mjipe huo ushauri”.

Harmonize na Wolper tangu wameachana kila mtu ameendeelea na maisha yake kwani Wolper ana mpenzi mpya anayejulikana kama Brown na Harmonize yupo na mpenzi wake mpya Sarah lakini tangu wameachana wawili  hao wamekuwa wakirushiana vijembe vya hapa na pale huku kila mtu akimtuhumu mwezie kwa kutokuwa mwaminifu kwenye mapenzi yao.

Comments

 1. catherine mpunga : September 13, 2017 at 10:45 am

  Mwelewe huyo pimbi,bila kukutaja wewe hawezi kukiki

 2. catherine mpunga : September 13, 2017 at 10:46 am

  Tanzania ya leo,mahusiano balaa,HARMONIZE ukiachwa achika blaza

 3. Nlijua yatafikia hapa,ila Wolper sasa tafuta mtu mzima utulie,hawa watoto watakuumiza bure

 4. Victoria Kavuri : September 13, 2017 at 10:49 am

  WCB inashuka kama mwendokasi, hizi story zimekua nyingi sana

 5. Ni uchungu sana,Wolper wapotezee mbali hawa madogo,watakutia presha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.