Loading...

Wolper: Sina wivu na Harmonize

July 17, 2017 at 15:20
Wolper: Sina wivu na Harmonize

Jacqueline Wolper hana machungu yoyote na mpenzi wake wa zamani – Harmonize. Mwigizaji huyo wa filamu za Bongo alisema kuwa aliachana na Harmonize miezi sita iliyopita. Alieza pia vitu vinavyo mvutia kwa mpenzi wake mpya – Brown.

“Tumeachana kama miezi sita hivi tulikuwa hatuelewani. Huyu BFF yaani Best Friend Forever tuna kama wiki hivi. Tulikutana vizuri tu alianza kuniona kama miaka minne hivi before. Kinachonivutia kwake ni mpole na mkweli, kwa hiyo ni rafiki yangu mzuri sana,” Wolper alisema kupitia kipindi cha The Weekend Chart Show ya Clouds TV.

Jacqueline Wolper na Brown

Wolper hata hivyo alisisitiza kuwa yeye na Brown ni marafiki tu wala sio wapenzi;

“Mimi siwezi kuingia kwenye vita na siwezi kuwa na uchungu japo stress hazifichiki na furaha haifichiki. Kwa hiyo nyie mnaweza mkajadili. Vitu vya instagram siyo vya kweli vyote japo wanakuwa na vitu vyao vina ukweli kidogo. Huyu kaachana na mtu wake miezi miwili halafu mwezi wa tatu tukakutana. Kwa hiyo, hizo ni story tu wote tumekutana single ila tofautisha wale ni wapenzi na sisi ni BFF na tupo serious. Ni marafiki wa kweli. Mimi siyo mtu wa TV naye siyo mtu wa TV.”

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere