“Wote Wanaomkejeli Ruge Hawatamaliza Mwaka”- Mwijaku

Muigizaji maarufu wa Bongo movie Mwijaku amewajia juu watu wote ambao wamekuwa wakimkejeli aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi Ruge Mutahaba.

Baada ya Ruge kufariki siku mbili zilizopita maneno Mengi yaliibuka kwenye Mitandao ya kijamii ikiwemo Msanii kama Dudubaya ambaye alianza kumuongelea vibaya Marehemu.

download latest music    

Baada ya watu Mbali Mbali kukemea Suala hilo Serikali imeingilia kati na sasa Hivi Msanii Dudubaya amewekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa muda usiojulikana.

Mwijaku amewajia juu watu wote wanaomsema vibaya Marehemu Ruge na kusema wazi kuwa yeye binafsi ana mpango wa kusali na kuwaombea dua watu wote ambao wanafanya matendo hayo na kuhakikisha kuwa watu hao hawatamaliza mwaka:

Naomba niseme kuwa mimi binafsi nitafunga na kusali na kufanya dua kwa ajili ya wote ambao wamekuwa wakimdhihaki Boss Ruge.

Mimi Ruge ni Kaka yangu kwaiyo hiyo Dua naapa itawafikia hao watu na ninawahakikishia hao watu kuwa huu mwaka hawataumaliza “.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.