Yawezekana Haya Ndio Yaliyomtoa Zari kwa Diamond.

Ikiwa inakaribia wiki sasa tangu mwanamama Zarina Hassan  kuandika ujumbe mzito ulioibua hisia kali kwa mashabiki wa muziki wa bongo  baada ya kuandika rasmi kuwa anaachana na uhusiano wa kimapenzi alikuwa nao na mwanaume wake aliyezaa nae watoto wawili ambae pia ni msanii mkubwa na maarufu bongo na nje ya bongo Diamond Platinumz.

Pamoja na kwamba hakuna alichojibu mwanaume huyo baada ya kuachiwa kwa ujumbe huo na mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa instagram siku ya wapendanao lakini hisia za mashabiki zimekuwa kali juu ya  kuachana kwa wawili hao.Wapo walianza kuangalia kwa upande wa pili sababu ndogo ndogo ambazo zinawezekana zilikuwa zikimsumbua mwanamama huyo kwa muda mrefu , huku wachambuzi wa mapenzi wakisema kuwa katika mahusiano kitu chochote kidogo kinapokuwa kinajirudia rudia huweza kuwa kikwazo kikubwa.

download latest music    

Uwepo wa skendo nyingi za kuwa na wanawake, kila kukicha katika mitandao kumekuwa na sababu za kuchepuka kwa Diamond na wanawake tofauti tofauti ambapo kwa mwanamke wa kawaida anaweza kuchoka kusikiliza kila siku swala la mwanaume wake kuwa na wanawake wa aina tofauti tofauti tena wasioweza kulinganishwa nae kwa kitu chochote.

Ukaribu wa Wema Sepetu na Diamond uliozuka hivi karibuni,Diamond na Wema walikuwa mahasimu wakubwa baada ya kuachana na sababu moja wapo ya Dai kuachana na wema ni Zari,hivyo inampa Zari wakati mgumu kukubali tena kuoana wawili hao wapo karibu ilhali mwanamke huyo alishakuwa na  mapenzi na mume wake kabla.

Jambo lingine linalosemekana kuachana kwa wawili hao ni kukosekana kwa watu wa karibu hasa wakubwa ambao wangeweza kuwa na msaada katika kuwashauri swala zima la mahusiano , tena ukizingatia kuwa Zari hana wazazi wote wawili hivyo hakuwa na maamuzi ya busara kutoka kwa watu wakubwa wa kumshauri huku upande wa Diamond wazazi wake hasa mama amekuwa ni mtu wa  kukubali maamuzi ya mtoto wake.

Jambo lingine ni utajiri wa Zari,mwanamama huyo anahela kiasi kwamba anachotaka kutoka kwa Diamond ni mapezni ya kweli na sio cha zaidi, hivyo Zari anaonekana kuchoshwa na drama za kila siku kutoka kwa Diamond ilhali kwake alikuwa akitafuta upendo wa kweli na sio pesa kama wanawake wanaotembea na mzazi mwenzie wanavyotaka.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.