Young D- Nisifananishwe na Msanii yoyote yule

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Daresalaam amesema asifananishwe wala kushindanishwa na vidagaa lwa kitu chochote kile, iwe kifedha, kimuziki, kimavazi na hata kwa wasichana wakali.

Young D akiwa no miongoni mwa vivutio kwa watu wengi kutokana na umri wake mdogo na hata kwa staili zake za kuimba amewajia juu wale watu wote wanamfananisha na wasaani wenzake wenye sifa sawa kama umri, aina ya mziki wanaoimba na hata manjonjo yao.

download latest music    

Wasanii kama Dogo janja ambaye ana ufanano mkubwa na Young D kutokana wawili hao kuanza kufanya sanaa hii ya muziki wakiwa watoto wadogo mpaka leo kuwa vijana wakubwa ambayo hali hiyo imewapelekea mashabiki kuwafananisha na hata kuwashindanisha.

Young D amedai hayo huku akisisitiza kuwa yeye ni bora kwa upekee wake aliokuwa nao katika kufanya sanaa yake hivyo watu wasimfananishe na wasanii wengine kwani haendani nao kama mashabiki wanavyodai.

Young D ambaye mapema mwaka huu aliingia katika skendo ya kutumia madawa ya kulevya, lakini baadae alikiri kupata msaada na sasa anendelea vizuri na saivi ngoma yake ya Kiutani utani inatamba katika stesheni mbalimbali za redio.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.