Young Dee Aliniita Nikampelekee Chakula Nikamkuta Na Mwanamke- Amber lulu

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber lulu amefunguka na kueleza moja kati ya matukio yaliyomuumiza kwenye uhusiano wake na msanii mwenzake Young Dee ambapo amedai ameshawahi kumfumania na mwanamke mwingine ndani.

Amber lulu amekuwa muwazi sana kila inapokuja kwenye hisia zake na Young Dee kwani ni  mara kwa mara ameweka wazi kuwa ampenda sana hata Kama amemuumiza sana kwa kuchepuka na wanawake wengine.

download latest music    

Amber lulu amekiri kuwa pamoja na kwamba yupo na Prezzo lakini Young dee ni moja Kati ya mwanaume ambaye alimpenda sana lakini pia amekiri kuwa tukio ambalo hatokuja kulisahau kwenye maisha yake ni siku ambayo Kwani alimfumania live.

Kwenye interview aliyofanya na East Africa redio kupitia kipindi cha Planet Bongo, Amber lulu alifunguka mengi:

Yaani hata leo hii Young Dee akimposti demu mwingine Instagram mimi naumia ingawa siwezi kumkataza lakini pia ikitokea nimeachana na Prezzo naweza nikarudiana naye ingawa ameniumiza sana kipindi cha nyuma kama nakumbuka kuna Siku alinipigia Simu akaniambia yuko studio somewhere akaniambia hebu my baby nipikie kile chakula ninachokipendaga ambacho kilikuwa ni ugali na maini basi mwenyewe nikjipikilisha pale unyamwezi pembeni nimemaliza nimebeba kile chakula nimpelekee alikuwa kwenye hoteli Fulani hivii kufika pale namkuta na msichana mwingine kusema kweli niliumia sana”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.