Loading…

Young Killer Ametaja Kitu Kilichomuumiza Zaidi Kuhusiana na Harusi Ya Dogo Janja

November 14, 2017 at 10:13

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Young Killer Msidoki amejiri kuwa amesikitishwa sana kwa kitendo cha yeye kutokuchangia kwenye harusi ya rafiki yake Dogo Janja.

Harusi ya Dogo Janja na Irene Uwoya iliwashtua watu wengi wiki chache zilizopita huku watu wengi wakibaki midomo wazi kutokana na tofauti kubwa iliyopo baina yao ya kiumri.

Loading...

Kwenye mahojiano Young Killer aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa amekiri kuwa ameumia kuwa hajachangia kwenye harusi ya janjaro:

Kilichoniuma zaidi ni kwa nini sijachangia harusi ya mwanangu hicho ndio kilicho-nipain lakini all in all nimefurahi kwamba janjaro ameoa kwa kweli ni kitu kikubwa sana kwa upande wake ni lazima apate furaha yake, kile kitu kinachomfanya awe na furaha lazima akifanye ili maisha mengine yaweze kuendelea lakini mimi pia ni mtu ambaye nilikuwa sijui nini kilikuwa kinaendelea nilijua kama watu wengine walivyojua nilikuwa surprised kuhusiana na harusi lakini nilikuwa nafahamu kuwa walikuwa na mahusiano”.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ya kwamba Dogo Janja, Young Killer na Young Dee wana bifu na hawapatani lakini Young Killer amekataa kuwa na bifu Dogo Janja:

Dogo Janja mimi ni mwanangu na tumekuwa tukizungumza vitu vingi kwaiyo nilikuwa nafahamu kuhusu uhusiano wake na Uwoya lakini sikujua kuhusu ndoa lakini nakumbuka baada ya ndoa alinitafuta mwenyewe na kunipa taarifa”.

 

Comments

  1. Waacheni waoane bwana ndoa tamu wanasemaga

  2. Ni sawa sio lazma watu wajue kila mpango

  3. Hata mimi nlishangaa ila ishafanyika

  4. Janja aliwashangaza wengi sana

  5. Uwoya mzuri mwacheni dogo ale bata

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.