Young Killer Athibitisha Kuachana na Miss Hip-Hop

Mwaka 2016 msanii wa musiki bongo  Young Killer wa Msodoki alitangaza kumuoa mwanamke aliyesema kuwa yuko nae katika mahusiano aliyekuwa akijulikana kama miss hip-hop, hali iliyofikia mpaka kumpachika jina ilo la miss hip-hop ikiwa kama ishara ya kuonyesha ni jinsi gani wamekuwa wakipendana.

Hata hivyo msanii huyo amefunguka hivi karibuni na kusema kuwa kwa sasa hayuko katika mahusiano ya kimapezni  na mwanadada huyo  tena kwaio maswala ya ndoa tayari yalishavunjika na hayupo katika mahusiano na miss hip hop  kwa takribani miezi sita sasa ilikwisha pita.

download latest music    

kulikuwa na kutokuelewana kidogo kati yangu na yeye swala lilipopelekea tusiwe pamoja kwa takribani miezi sita sasa. -Aliongea Young Killer

Akiongezea kwa kufafanua zaidi msanii huyo amesema kuwa sio swala la usaliti  hata kidogo lilowafanya waachane ila ni sababu za ndani ambazo hawezi kuziongelea zilizowafanya waachane.

Young Killer tangu alipotangaza yuko katika mahusiano na miss hip-hop , hajawahi kupata skendo yoyote ya kimapenzi na ndio maana hata walipoachana ilikuwa ni vigumu kujua kwa sababu ni moja ya wasanii waliaoamua kuweka mahusiano yao ya kimapenzi kuwa ni siri  zao katika maisha.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.