Young Killer: Siwezi Kubadilisha Muziki Ninaofanya

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Erick Msodoki maarufu kama Young KIller ameibuka na kuweka wazi kuwa hana mpango ya kubadilisha muziki anaofanya.

Sio siri kwenye gemu la Bongo fleva imeonekana wazi kabisa kwa miaka ya hivi karibuni muziki unaopewa nafasi na wenye soko zaidi ni muziki wa taratibu ile RnB na mziki wa Hip Hop umeonekana kulega lega kidogo.

download latest music    

Mara kadhaa Young KIller amekuwa akipewa ushauri na mashabiki zake wanataka abadilishe aina ya kuchana ili aweze kuangalia kama mziki wake utapata soko zaidi katika upande mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes, Young KIller amesisitiza kuwa hawezi kubadilisha aina ya muziki anaofanya kwani ndio muziki uliompa mafanikio mpaka leo anajulikana kwa mashabiki zake:

Sasa hapo nibadilike nini. Mtu unayepata shoo nyingi inaonesha wazi kwamba unakubalika. Siwezi kubadilika na nitaendelea kukimbiza zaidi na zaidi“.

Hivi sasa Young Killer anafanya vizuri na wimbo wake wa Shots aliomshirikisha rapa mkali kutoka 254 Kenya anayeitwa Khaligraph.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.