Loading...

Zamaradi Ashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Ruge, Amsifia kuwa Baba Bora.

February 22, 2019 at 10:20
Zamaradi Ashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Ruge, Amsifia kuwa Baba Bora.

Mzazi mwenza wa mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mtahaba ‘Zamaradi Mketema amefunguka na kueleza kuwa Ruge ni mtu ambae hamtupi mtu hasa akiwa kwenye matatizo.
Akifanya mahojiano Zamaradi amesema mtu wa karibu na Ruge alimpa taarifa ya hali ya Ruge kwa sasa, Ifahamike kuwa kwa sasa hali ya Bwana Ruge Mutahaba haiko sawa na bado yupo nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Akiongea katika 360 ya Clouds media , zamaradi anasema kuwa pamoja na kwamba wao wa sasa hawako pamoja lakini hawezi kuacha kusema kuwa Ruge ni moja ya baba bora kwa watoto wake na kwenye swala la malezi , na wala hawezi kuacha kuwajua hali watoto wae kila mara.

Loading...

hata hivyo zamaradi anasema uwa kila mara ameuwa akiwasisitiza watoto wake kuwa wanamuombea baba yao hasa kwa  kipindi  ambacho ni mgonjwa na anahitaji maombi sana li aweze kuwa sawa.

zamaradi anasema anaungana na kila mmoja mwenye nia ya dhati ilikufana kila linalowezekana kwa ajili ya kupata pesa za matibabu ya baba watoto wake huyo.

Hata hivyo zamaradi amefungukia ukweli wa jinsi walivyoanza mahusiano Zamaradi amesema “Tulikutana na Ruge kwenye mazingira ya kazi, na mimi nimemjua Ruge kupitia Babu Tale,Tale ndio mtu ambaye alinitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza, alinipa namba yake akanimbia mtafute huyu bwana lakini usimwambie kama mimi ndiye niliyekupa namba” alisema Zamaradi

Share

Comments

  1. R.I.P braza mungu akupunguzie adhabu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…