Loading...

Zari abadilisha jina la mtoto wake wa kike Tiffah

July 13, 2017 at 15:53
Zari abadilisha jina la mtoto wake wa kike Tiffah

Kifungua mimba wa Diamond amebadilishwa jina na kupewa jina la mamake, Zari alidhibitisha haya kwenye mtandao wa Instagram.

Mtoto wa kike wa Diamond anajulikana kama Tiffah Dangote, jina hilo la pili ni ya babake ambaye alijibandika ‘Dangote’ kwasababu ya mafanikio yake kimuziki.

Hata hivyo Zari aliwajulisha watu kwa Tiffah sasa anaitwa Tiffah Hassan na sio Tiffah Dangote. Alisema hayo kwenye comment section kwa Instagram baada ya mtu kuita mtoto wake Tiffah Dangote.

Hatua ya Zari kubadilisha mwanawe jina umezua uvumi kuwa Zari amekosana na Diamond ndo sababu aliamua kutoa jina la Diamond (Dangote) na kumpa jina yake (jina Hassan).

Wambeya wanasema kuwa Diamond na Zari walikosana kwasababu Simba hajaenda kumwona mama mkwe wake ambaye alilazwa hospitalini huko Afrika Kusini. Na mbaka sasa Diamond hajamtumia mama mkwe wake salamu za heri.

 

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere