Zari adaiwa kupungua mwili Kisa na sababu, Hamisa Mobetto

Image: Zari

Mrembo na mama watoto wa Diamond Platnumz, Zari Hassan anasemekana kuwa na mawazo mengi ambayo yamemfanya kupungua kimwili sababu ya kufikiria sana.

Habari hizi ziliwekwa wazi na chanzo kimoja kilichozungumza na Global Publisherz kueleza hali ya Zari inavyoendelea tangu Hamisa Mobetto kuweka wazi kuwa Abdul Naseeb ni mtoto wa Diamond Platnumz. Chanzo hicho kilisema;

download latest music    

“Zari kapungua mwili kweli jamani. Mobeto amemponza. Amemsababishia watu wamtukane sana Zari kiasi ambacho amekosa amani kabisa. Masikini mtoto wa watu kakonda kweli sasa hivi.Ukitazama picha za Zari sasa hivi si Zari yule aliyetoka kujifungua. Tena kwa kawaida tunajua mtu ukitoka kujifungua unanenepa lakini kwa Zari mambo yamekuwa tofauti. Ngoja niwatumie picha yake ya sasa muone,”

 

Hata hivyo maneno haya yanauwezekano ya kuwa ya kweli kwani kwenye picha za Sasa, Zari anaonekana kupugua mwili sana.

 

 

Zari
Zari

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua