Zari ajibu tetesi za Diamond kutoka na Dilish.

Image: Zari

Kumezuka kwa tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano mpya wa kimapenzi  kati ya msanii mkubwa kutoka Tanzania  Diamond platnumz na mrembo kutoka nchini Namibia ambae pia alishawahi kushinda shindano la Big Brother The Chase mwaka 2013 Dilish Mathew ,ambapo wawili hao walitumia mitandao yao ya snapchat kutuma baadhi ya picha na video zinazosadikika   kuwa walikuwa pamoja visiwani Zanzibar na walionekana kufikia hoteli moja na hata kupanda ndege moja wakati wa kurudi.Hata hivyo kimepita kimya kwa muda  bila hata mmoja kati ya wawili hao kuongea chochote.

Kupitia snapchat yake,Zari  aliamua kujibu tuhuma na tetesi hizo huku akionyesha kutokujali kabisa kuhusu maneno hayo na anasema yuko busy na kutafuta ela ‘Oh u dming to tell me how he cheated,…?so many just like so many on market.. like why do people think it all about fightin for..,’ ameandika Zari akimaanisha kuwa kwa upande wake hafikirii kugombania mwanaume , na watu wasikae kumsumbua kumtumia sms kuhusu mumewe anavyotemba na wanawake wengine.

download latest music    

Zari anasema kuwa katika vitu anavyoweweza kugombania kwa sasa ni ela na si kitu kingine,”honey i will fight for 1m not ..closed a deal worth this week “aliandika zari kwa kuongezea .

Zari amemtaja Ivan ,ambae alikuwa mumewe hapo awali , mumewe wa kwanza aliezaa nae watoto wa tatu kabla ya kukutana na diamond , Ivan ambae hivi sasa ni marehemu alifariki miezi michache , zari aliongezea kwa kusema kuwa Ivan amemuachi urithi mwingi ivyo hana haja ya kuangaika,”heading to my bed now, i dont get bedded for busness class ticket ,Ivan built a legacy for me that i can afford that any day , any time”

Zari na Diamond ni wazazi wa watoto wawili Tiffah na Prince Nillan ,wawili hao wamekuwa na skendo nyingi tangu kuanza kwa mahusiano yao, hata hivyo kumekuwa na tuhuma nyingi sana zinazosambaa zinazomtuhumu diamond kutoka na wadada tofauti na hivi juzi alikumbwa na kashfa ya kukataa mtoto wa kiume aliyezaliwa na video queen maarufu Hamisa Mobeto

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.