Zari amjia juu mzazi mwenzie

Ikiwa hata interview haijaisha kati ya Diamond na kituo cha habari cha Clouds Media Zari amjibu mzazi mwenzie kuhusu yale aliyokuwa anayasema leo katika interview iyo.Diamond ambae leo ameamua kusema ukweli kuhusu tetesi zilizokuwa zinasambaa mitandaoni juu ya mtoto wa video quen Hamisa Mobeto .

Diamond amekiri kuwa alitembea na Hamisa na amepata mtoto nae  na kusema kuwa alishaongea na mzazi mwenzie (Zari) na kwamba mama wa watoto wake yuko sawa na walishayamaliza lakini Zari ameonekana kupinga maneno hayo .

download latest music    

Katika ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika “haha… u playing yourself ..the lies telling about me knowing about your side chic..try and fix your mess and stop  with lies .Me being quite doesnt mean am stupid .Be very careful with your words’ aliandika zari akikanusha kuwa kitendo cha Daimond kusema kwa yeye alikuwa anajua juu ya yeye kuwa na mahusiano na Hamisa ni uongo.

Hata hivyo Zari anaongezea na kusema kuwa  kitendo cha yeye kukaa kimya ni kwa sababu yeye ni mama wa watoto wake ” i may be the mother of your kids  and that’s the reason am keeping silence &respect. You might want to Google about ‘Defarmation of character law suit’ Dont try me” aliandika Zari

Majibu haya yamekuja baada ya Diamond kukubali na kuomba msamaha kuhusu ukweli kuwa mtoto alizaliwa kwa Hamisa Mobeto ni wakwake lakini alikaa kimya ili kuweka kwanza mambo sawa ndipo atangaze.

Akiwa bado katika  mahujiano Diamond aliulizwa kuhusu maneno hayo aliyopost mama wa watoto wake , na alijibu hivi “Anavyosema hivyo namuelewa  anachokizungumza,najua hawezi kuwa sawa kwa muda huu, lakini pia yapo baadhi ya mambo nimeyazungumza hapa  ,  hakuwahi kuyasikia.” alipoulizwa ni mambo gani alijibu vitu kama ela za matumizi , kumnunulia gari Hamisa ni vitu ambavyo hakuwahi kumwambia Zari ivyo ana haki ya kuijsikia vibaya.

Zari na Diamond  wamekuwa katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitatu na wamefanikiwa kupata watoto wawili wakike moja na kiume mmoja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.