Loading...

Zari Atangaza Zawadi Kwa Mashabiki Zake Uganda

November 09, 2018 at 07:19
Zari Atangaza Zawadi Kwa Mashabiki Zake Uganda

Mwanamama mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda na Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ametoa  zawadi Nono kwa mashabiki zake nchini Uganda.

Zari ameyafanya hayo muda mfupi baada ya kupata zali la kuwepo katika vivutio vikubwa vya utalii nchini humo akiwa kama balozi wa utalii ambapo atatembelea katika mbuga kubwa za wanyama pamoja na chanzo cha Mto Nile pande za Jinja.

Loading...

Akizungumzia ishu hiyo ndani ya Hoteli ya Serena nchini Uganda, Zari alisema ili kuwavutia watalii na watu wengine ameona kuwa na kampeni maalum ya kuwashirikisha mashabiki wake na kampeni hiyo ameiita jina la Tulambule Ne Zari akimaanisha Tutembee Na Zari.

Niambie sehemu unayopenda kutembelea Uganda, unaweza ‘ku-google’ vivutio vyote vya utalii Uganda na ukasema ni sehemu gani unapenda kutembelea,” alisema Zari na kuongeza: “Nitatoa ofa ya gharama zote za safari na ujue tu mimi ni Boss Lady kwako na kwa mwenzako au familia yako”.

Hili ni moja tu Kati ya madili  ambayo Zari  amekuwa akiyapiga tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz Lakini pia Kumekuwa na tetesi za ubalozi wa nchi unaoweza kumuangukia mrembo huyo.

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
5 Comment authors
TatianaYasminWhite NegroZarinaMoni Recent comment authors
newest oldest most voted
Moni
Guest
Moni

Nice…

Zarina
Guest
Zarina

Unafaa ubalozi sasa

White Negro
Guest
White Negro

Keep stunting on them

Yasmin
Guest
Yasmin

👏👏👏

Tatiana
Guest
Tatiana

Najua unajipendekeza upate ubalozi….


in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.