Babake mzazi na Belle 9 afariki dunia baada ya kugongwa na boda boda

Mzazi na Bella 9 wamem[poteza baba yao baada ya kugongwa na boda boda kama ilivyoripotiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Mzee Damian anasemekana kuwa aligogwa na boda boda iliyomuacha akiwa hali mahututi. Hata hivyo mzee huyu alifariki dunia usiku wa kuamkia leo kulingana na alichosema Jah Zamba ambaye ni meneja wa Mzazi.

download latest music    

Ajali hii ilitokea mjini Morogoro alikokuwa akiishi. Kulingana na Bongo 5 mzee Damian alivunja mguu mmoja na kuumia vibaya baada ya ajali hiyo.

Ata baada ya kupelekwa hospitali madaktari hawakuwa na njia yoyote ya kumsaidia. Alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi lakini hawakuwa na dawa zilizokuwa zinahitajika kumtibu mzee huyu. Hata hivyo dereva wa boda boda hiyo pia aliumia vibaya baada ya taya kuvunjika na kumjeri kichwa.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua