Dogo Janja: Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi

Dogo Janja amesema kuwa anamkubali Harmorapa hata kama watu wengi wameongea matope kumhusu. Rapa huyo chipukizi amewaudhi watu wengi kwa vitendo na muziki wake.

Soma pia: Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

download latest music    

Akiongea katika kipindi cha eNewz, Dogo Janja alisema kuwa anamkubali Harmorapa kwasababu ameonyesha uthubutu katika muziki licha ya watu kumkatisha tamaa.

Msanii huyo wa Bongo fleva aliongezea kuwa Harmorapa anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka ili muziki wake ukubalike kote.

Harmorapa

“Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi kama mimi ….Ni mtu ambaye amejaribu kuonesha uthubutu..Step ambayo ameenda ndiyo imenifanya mimi nimkubali zaidi, alianza wimbo wa kwanza watu wakamtisha tamaa, vunja moyo lakini hakuvunjika moyo. ‘Dude’ la pili akajaribu halafu likawa kali mimi nikasema huyu anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka kwa kuwa anaonekana na moyo wa uthubutu na anapenda kujifunza zaidi” alisema Dogo Janja.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere