Hamisa Mobetto aendelea kudai kuwa maisha yake na ya Abdul Naseeb yako mashakani

Image: Hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto anaendelea kuhofia kuwa maisha yake na mtoto wake aliyezaliwa Agosti 8, mwaka huu.

Kulingana na marafiki wake wa karibu, Hamisa Mobetto anaishi na wasiwasi kutokana na vitisho anazozipata kila siku kutoka kwa baba ya mtoto wake. Chanzo kimoja kutoka familia ya Hamisa kilisema;

download latest music    

“Unajua baada tu ya kujifungua kulienea habari nyingi kuwa mtoto huyo ni wa msanii huyo hasa baada ya Hamisa kumpa mwanaye jina hilo. Kilichofuata, kwanza msanii huyo alikimbilia kwenye media (vyombo cha habari) kukanusha habari hizo ambazo zimekuwa zikizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu. Unajua jamaa (msanii huyo) alidhani kuna siri chini ya jua kuwa anaweza kuficha jambo hilo maana watu walikuwa wakimchomea kwa mpenzi wake ambaye amezaa naye.

Aliendelea kusema,

“Ili kumziba mdomo Hamisa, msanii huyo aliona ni bora amkane mapema lakini Hamisa siyo wa mchezomchezo maana aligoma kuficha ishu hiyo. Baada ya kuona anaweza akabumburua ishu, msanii huyo alimpiga biti asizungumze na vyombo vya habari kabla ya kumwekea ulinzi wa chinichini kuhakikisha waandishi hawamfikii Hamisa. Sehemu pekee ambayo Hamisa aliona jamaa huyo hawezi kumzuia ni kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Snapchat ‘so’ akawa anaposti vipande vya baadhi ya viungo vya mtoto huyo. Sasa baada ya kuona hivyo, msanii huyo ambaye alikwenda mara moja tu kumuona mtoto huyo alianza kumpigia simu na kumtumia meseji za vitisho. Wewe fikiria Hamisa na kichanga chake sasa anaishi kwa hofu maana jamaa amemuambia kama atafunguka kuwa amezaa naye atamuondoa uhai yeye na mtoto wake. Hali hiyo imeifanya family ya Mobeto iwe na hofu kubwa na ili kujiweka salama, aliona ni bora aende polisi kuripoti ili kama kutakuwa na jambo lolote baya litakalomkuta yeye na mwanaye, basi mhusika atakuwa ni msanii huyo. Mwanzoni tulidhani ni ishu ndogo lakini kwa vitisho anavyopokea Hamisa, vinamnyima raha na kumfanya alie tu.

Akaongeza kuwa…

Hamisa Mobetto na mwanae
Hamisa Mobetto na mwanae

“Kiukweli Hamisa anatia huruma sana na anahitaji msaada kwa sababu mbali na msanii huyo pia anapata vitisho kutoka kwa mpenzi wa jamaa huyo. Sasa watu wanajiuliza, wakati anatembea naye hakujua kuwa kinaweza kupatikana kiumbe? Na kwa ustaa wake anashindwa nini kulihendo suala hilo kwa busara ili lisimchafulie kuliko kutoa vitisho hivyo?” kilifunguka chanzo chetu hicho na kuongeza. Hata kwenye ukurasa wake wa Snapchat, Hamisa ameshatahadharisha juu ya kutishiwa kuuawa yeye na mwanaye.”
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa liliperuzi kwenye ukurasa wake huo na kukutana na ujumbe wa Hamisa uliosomeka:
“Mlidhani atafia tumboni enh…au mlijua nitafia leba…. nyie siyo Mungu na hamtakaa kuwa kamwe…& if anything bad and I mean anything bad happens to me or my son hatutawaacha salama!!!”

 

Hamisa na yeye aka sema;

‘MIMI NA MWANANGU TUNAUAWA WAKATI WOWOTE’ Ni kweli mimi na mwanangu tunauawa muda wowote. Nina ushahidi wa kutosha wa vitisho so nimeona ni vyema nitoe taarifa kwenye vyombo vya usalama,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua