Hawa watarudiana tu! Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva Shilole apatikana akiwa katika mapozi ya kimapenzi na ex wake

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliachana na mpenzi wake Nuh Mziwanda karibu miaka mitatu iliopita. Shilole alidai kuwa wivu ndiyo uliosababisha yeye na mchumba wake kuachana.

Shilole na Nuh walijibizana kwa maneno mazito mazito kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kuachana.

download latest music    

Lakini sasa dalili zaonyesha Shilole and Nuh wako tayari kurudiana. Hii ni baada za picha zinazowaonesha wakiwa pamoja katika mapozi ya kimapenzi kutokea kwenye mitandao ya kijamii.

Shilole ata hivyo amewataka watu kuacha tabia ya kueneza uvumi baina yake na Nuh Mziwanda, msanii huyo anasema watu ndiyo wanavumisha habari potovu kumhusu yeye na Nuh.

“Mimi na Nuh ni washikaji tu, halafu Mwanza hatujakatana katika ‘show’ ila kila mtu alikuwa kwenye mishe zake hivyo sijaona tatizo la mimi kusalimiana naye pamoja na kupiga picha kwa kuwa alikuwa ‘Ex boyfriend’ wangu na nimeishia naye takribani miaka 5 watu waache tabia ya kukuza vitu ambavyo hawana uhakika navyo”. Alisema Shilole kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere