Jacqueline Wolper afunguka kuhusu unafiki unaolemaza filamu za Bongo

Washikadau katika filamu za Bongomovies ndo wanaochangia kuzorota kwa hali ya mambo katika sekta hio ya uigizaji – Jacqueline Wolper ameeleza.

Mrembo huyo anasema kuwa anakerwa sana na unafiki wa wasanii, anadai kuwa uigizaji nchini umelemazwa na unafiki.

download latest music    
Jacqueline Wolper

“Nachukizwa na unafiki Bongo Movi, kwa kweli unakera sana, hawako kiualisia ndiyo maana kufika tunapotaka ni ngumu sana,” Wolper alisema akizungumza na Showbiz wakati wa maandamano ya kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji na uuzwaji holela wa sinema za nje.

Wolper alisema kuwa wasanii wangekuwa na umoja wangeungana siku hiyo na kuweza kutoa mwelekeo mmoja ambao ugechangia malalamika yao kuskizwa.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere