Jacqueline Wolper afunguka kwanini ameshindwa kuvuka ‘border’

Watu wengi watakubali kuwa Jacqueline Wolper ni muigizaji mwenye kipaji kikubwa, lazini mrembo huyo ameshindwa kufanya filamu za kushirikiana na wasanii wa nje.

Nini haswa ndo kikwazo kinachozuia Wolper kuvuka ‘border’? Lugha ya Kiingereza ndo sababu kubwa inayowafanya waigizaji wa Tanzania kushindwa kufanya filamu za kushirikiana na wasanii wa nje

download latest music    

Wolper alikiri kuwa Kiingereza ni tabu kwake, alisema kuwa kwa sasa ana mwalimu kwa ajili ya kuboresha kiingereza chake ili atimize ndoto zake za kucheza filamu na wasanii wa nje kwa lugha ya kiingereza.

“Wasanii wachache ndio wanaojitahidi kwenda kufanya kazi na wasanii wa nje, mimi na baadhi ya wasanii wengine hatuwezi kushirikiana na hao kwa kuwa hatujui Lugha ya Kiingereza kwa ufasaha kwa kuwa filamu nyingi huzungumzwa kiingereza,” alisema Wolper.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere