King Kiba atisha baada ya kuweka rekodi mpya YouTube

Image: Alikiba

Alikiba ama ukipenda King Kiba ameweka rekodi mpya Afrika Mashariki kama msanii ambaye video yake imepata kutazamwa na watu milioni masaa 38 baada ya kuiwachia.

download latest music    

Seduce me imeweka rekodi ya kipekee ambayo hata wakalik ama Diamond Platnumz na Vanessa Mdee bado hawajaweza kufikisha. Kupitia ukurasa wake wa instagram, King Kiba aliweka post akiwashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha kuvunja rekodi hiyo. Aliandika;

“Ahsanteni sana kwa upendo, nisingebarikiwa zaidi na kupendelewa bila nyinyi, nyinyi ni wa maana sana kwangu na nafanya haya kwa ajili yenu”,

kampuni ya Rockstar ambayo inamsimamia Kiba pia iliandika ujumbe kusema kuwa wimbo huu umevunja rekodi ya kipekee na ni video zinazotrend Tanzania na Kenya.

“Historia ya kunjwa rekodi imewekwa, Mfalme Kiba na wimbo wake mpya wa ‘Seduce me‘ umekuwa wa kwanza na kipee kwa msanii wa Afrika Mashariki kufikia kutazamwa mara milioni 1 kwenye Vevo/YouTube ndani ya masaa 38 tu, ina ‘trend’namba 1 Tanzania na namba 1 Kenya kwa ‘weekend’ nzima, rekodi imevunjwa.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua