Kwanini Wanaume Wengi Wanaongoza kwa Kusaliti.

Ni ukweli mchungu ambao ni lazima tujadiliane kuhusu namna ya kuukomesha. Utafiti usio rasmi, unaonesha kwamba japokuwa wanawake na wanaume wote wanasaliti, lakini idadi ya wanaume wanaosaliti ni kubwa zaidi kuliko wanawake.

Kabla ya kujua sababu hizo, ni vizuri ieleweke kwamba katika kila usaliti unaotokea, kuna mambo mawili yaliyosababisha; matatizo katika uhusiano wa kimapenzi au matatizo ya mtu binafsi.

download latest music    

Kama tunakubaliana katika hilo, hebu kila mmoja ajiulize, kwa nini wanaume wanaongoza kwa usaliti? Kwa nini wanaume wanawasaliti wake zao? Wanawake ambao wanafanya kila kitu kwa ajili yao?

TENDO LA NDOA

Sababu kubwa inayofanya wanaume kuchepuka, ni kukidhi tamaa zao za kimwili. Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa masuala ya kimapenzi, Dk Tamy Wilson wa nchini Marekani, unaonesha kwamba wanaume ambao wanatimiziwa haja zao za kimwili mara kwa mara bila vikwazo, wana nafasi ndogo ya kusaliti ukilinganisha na wale wanaopata haki ya ndoa kwa ‘mbinde’. Kwa jinsi miili ya wanaume ilivyoumbwa, kadiri mtu anavyokaa muda mrefu bila kushiriki tendo, ndivyo tamaa za kimwili zinavyo ongezeka na kama akishindwa kuwa makini, anaweza hata kutembea na hausigeli ‘mchafu’ wakati ndani anaishi na mke mrembo mwenye sifa zote.

TABIA MBAYA

Ukiachana na wale ambao wanasaliti kwa sababu hawana jinsi, lipo kundi lingine la wanaume ambao kihulka wana tabia mbaya tu! Atapewa kila anachokihitaji kwa mkewe, atahudumiwa kimwili, kiakili na kihisia lakini kwa sababu ana tabia ya kupenda kudanganya, kufanya mambo kwa siri na kukosa uaminifu, atasaliti tu.

Watu wa namna hii wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia na mara nyingi, huwa hawadumu katika uhusiano hata mwanamke awe mvumilivu kiasi gani.

KUKOSA KUJIAMINI

Sababu nyingine inayofanya wanaume wawe na tabia ya kusaliti mara kwa mara, ni kukosa kujiamini.

Anaishi na mke au mpenzi mwenye sifa zote nzuri lakini moyoni mwake hajiamini, anahisi ipo siku mwanamke atamkimbia na kwenda kwa wengine, kwa hiyo kukitokea ugomvi kidogo ndani, anakimbilia kutafuta mwanamke wa pembeni akijidanganya kwamba hata mkewe akimkimbia, atakuwepo wa kumfariji.

Yupo tayari hata kumpangia nyumba mchepuko ilimradi tu awe na sehemu ya kukimbilia inapotokea ameachana na mkewe.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.