Mahakama yatoa amri Agnes Masogange akamatwe tena

Video vixen wa bongo Agnes Gerald amejipata mashakani tena baada ya mahakama kutoa amri akamatwe kwa mara ya pili baada ya kutofika mahakamani kwa mara ya pili kesi.

Agnes ambaye hapo mbeleni alikosa kufika mahakamani wakati kesi yake ilikuwa ikitajwa amerudia kosa hili kwa mara ya pili baada ya kutofika mahakamani alipopangwa kutajiwa kesi yake.

Agnes
Agnes

download latest music    

Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ametoa amri hiyo baada ya Masogange na wakili wake kukosa kuwasili. Kwa kosa hili sasa hivi Agnes Masogange atakamatwa kwa kutofika mahakamani na kutotoa taarifa ya kilichofanya kutofika.

Muigizaji huyu ana mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua