Malkia wa filamu Shamsa Ford amaibisha mpenzi wake wa kitambo – Nay wa Mitego

Rapper Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameaibishwa hadhani na Shamsa Ford – mpenzi wake wa kitambo.

Apo awali ilisemekana kuwa Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapper Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20 2017.

Nay wa Mitego ndo alisemekana kuwa chanzo cha habari kuwa mpezi wake wa kitambo Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’

Shamsa Ford na Nay wa Mitego walipokua bado wanapendana

Malkia huyo wa filamu hata hivyo amemkana Nay wa Mitego na kumaibisha hadharani. Akiongea na Bongo 5, Shamsa Ford alisema kuwa hajui chochote kuhusu show hiyo kwasababu Nay wa Mitego hajawai mwambia lolote kuhusu show hilo.

“Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live. Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote,”alisema Shamsa Ford.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere