Mambo Ya Kufanya Ili Kuzuia Marafiki Kuingilia Mapenzi Yenu

Kwenye mapenzi ni vizuri kwa kila mmoja kuwa na marafiki nje ya Mahusiano hii itasaidia kupeana nafasi na kila mtu kupata muda wa kufanya mambo yake bila kufuatana fuatana na kubanana muda wote.

Hata hivyo kuna wakati  marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.

download latest music    

Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.

1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine 
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo.
Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe.
Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.

4. Kuwa na subira.
Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: 
Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.