Mastaa Wakongwe Waliokataa Kuchuja Katika Muziki

Kuna baadhi ya wasanii wa Bongo fleva ambao tangu waanze muziki mpaka sana ni zaid ya miaka ishirini lakini bado wanafanya vizuri katika  muziki na wamekuwa chachu kwa wasnii wadogo ambao ndio wanachipuka.Hawa wamekuwa mchango mkubwa sana katika kuukuza muziki huu.

1.Farid Kubanda -Fid q

Fid q alianza musiki miaka ya 200,akifanya vizuri huku akiwakilisha wasanii wanaotka Mwanza.aina ya muziki anaofanya ni HipHop.Nyimbo nzake ambazo zimeshafanya vizuri hadi sasa ni pamoja na Fid q, Mwanza Mwanza,Sihitaji Marafiki, I Am a Proffessional , Roho aliyomshirikisha Christian Bella ambao kidogo alifanya totauti na vile watu walivyomzoea na hivi sana anafanya vizuri na wimbo wake wa Fresh.

2.Mr.Blue

Mr.blue alianza kazi ya muziki akiwa mdogo sana na alifikia hatua ya kugombana hata na familia yake kwa sababu ya kazi ya muziki.Wimbo wa ‘tabasamu’ ni moja ya nyimbo zilizotamba sana enzi zake, nyimbo nyingine ni pamoja na Mapozi,Tilalila,Baki na mimi, Pamoja na Pesa .Mr blue mpaka sasa ni msanii anaependwa na amekuwa mfano wa wasanii wengine wengi.

3.Proffesa Jay

Jina lake halisi ni joseph haule,  alianza muziki mnamo mwaka 1994.kwa sasa anajihusisha na siasa na ni mbunge wa Mikumi kupitia chama cha upinzani Chadema,,lakini kazi ya ubunge haijamfanya kusimama kazi za muziki.Baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri ni pamoja na Zari la Mentali, Hapo vipi, Nikusaidiaje, Mtazamo.na Aluta Kontinua.Kwa bongo alikuwa akijulikana kama kaka mkuu wa muziki wa Bongo.

4.Dully Syskes

Miaka ya 1999 dully alianza musiki , ni moja kati ya wasanii waliokuwa wanapendwa sana Tanzani ana mpaka sasa Dully bado anafanya vizuri,wimbo wake wa hi! ndio uliomtambulisha zaidi katika muziki, baadae akaja na nyimbo kama Salome,Baby Candy, na Dhahabu.Hivi karibuni aliimba wimbo aliomshirkisha Harmonize kutoa Wcb uliitwa Inde.Bado yupo katika game na anafanya vizuri.

5.Ambwene Yesaya-AY

AY amekuwa akifanya vizuri sana katika rap tangu miaka ya 1996, huyu ni mmoja wa wasanii ambao kwa sasa wanafanya muziki lakin pia ni wajasiriamali wakubwa.Unapomuongelea AY basi uwezi kumuacha Mwana FA pia.

Nyimbo kama Habari ndo iyo, Nangoja ageuke, Yule, na Usije mjini zilifanya vizuri sana katika muziki kipindi icho.Ay pia aliimba nyimbo aliyomshirikisha msanii Diamond inayojulikana kama ‘zigo remix’.Hivi karibuni AY alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake anaetarajia kufunga nae ndoa.

6.Mwana FA

Mashabiki wanamwita Binamu, alianza muziki miaka kama  15 nyuma iliyopita,Mwana FA amekuwa karibu sana na AY , na ni marafiki wanaofanya kazi pamoja kwa muda mrefu, ameshatoa nyimbo kama Habari ndo iyo, Unanitega,Nangoja ageuke, Kiboko yangu aliyoimba na Ali Kiba pamoja na Dume Suruali aliomshirkisha Vannesa Mdee.

7.Lady Jay Dee

7

Wamekuwa wakimwita dada mkuu maana ndie msanii wa kike alieduumu muda mrefu katika game, alijulikana kama Anakonda, Binti machozi, Komando Jide,na mengine mengi.Alijulikana sana kwa nyimbo zake zenye kuibua hisia kama Machozi, Siwema, Usiuseme Moyo,Siku Hazigandi,hivi karibuni amekuja na nyimbo kama Ndi Ndi Ndi na I Miss U baadaa  ya kukaa kimya kidogo.Jay Dee alifunga ndoa lakini baadaye aliachana na mume wake huyo aliejulikana kama Gadner G Habash,Ana band pia ya muziki inayoitwa Machozi Band.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.