Matukio ya Kupokea na Kuaga Mwili wa Marehemu Ruge jijini Dar Es Salam

Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba Uliwasili siku ya Ijumaa na kupita maeneno mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na baade kupelekwa katika hospitali ya Lugalo.

Siku ya jumamosi , ulipelkwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuagwa na watu mbalimbali na kuupatia heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa na kupelekwa kijijini kwao BUKOBA  ambapo ndipo mwili huo utazikwa katika nyumba yake ya milele.

download latest music    

Ruge ameliza wengi na wengi wameumia na msiba huo , huku kila mmoja aamini kwa jinsi watu walivyojitokeza kwa ajili ya kuupokea na kuupoa heshima zake za mwisho kwa DAR  na hata ulipofika kwao BUKOBA.

Mwili wa Ruge ukiwasili na kushushwa Uwanja wa Taifa.

Mwili wa marehemu ukipita katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar.

jeneza la marehemu likiwa limewasili viwanja vya karimjee tayari kwa kuagwa.

Familia ya marehemu (watoto wake na wazazi wenzake na Ruge) wakiwa katika ukumbi wa Karimjee.

Mh Magufuli akitoa mkoo wa pole kwa wazazi wa marehemu.

Baadhi ya wasanii wa THT wakiwa katika majonzi wakiimba Nyimbo za kuombeleza.

Nandy ni moja ya wasanii waliopata fursa ya kuimba wimbo aliokuwa akiupenda marehemu lakini alishindwa kuendelea na mtoto wa marehemu alimsaidia kushuka jukwaani.

Barnaba alipokuwa akiongea machache kuhusu  baba yake Ruge na baada ya hapo alishindwa kuendelea na kuzimia.

Zamaradi mketema ambae ni mzazi mwenza na Ruge akiingia uwanjani hapo.

Baadhi ya wasanii wakiwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu.

Baadhi ya watu siku ya jumapili wakisubiri mwili wa marehemu Ruge kuwasili katika viwanja vya ndege  BUKOBA.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.