Mwala Adaiwa Kupagawa na Warembo Wa Bongo

Msanii mkongwe wa maigizo kutoka pande za Kenya Mwala amedaiwa kuonekana akiwa anajichanganya na warembo wa kibongo huku akiwa karibu na kupiga nao picha.

Mwala alikuwepo Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar kulipokuwa na tamasha la utoaji wa Tuzo za Kimataifa za SZIFF alionesha kudatiswa na warembo wa Kibongo waliokuwa wakimfuata kubadilishana naye mawazo na kupiga naye picha.

download latest music    

Katika tukio hilo ambapo msanii huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakikabidhi tuzo hizo, baada ya tukio hilo alipokwenda kukaa ndipo mademu wa Kibongo wakamiminika huku wengine wakililia ‘selfie’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers , Mwala alisema aliamua kujiachia na warembo wa kibongo kutokana na ushabiki wao katika kazi

Ukweli sikuwahi kujua kama nina mashabiki wengi hivi hapa nchini hivyo hali hii inanipa faraja ndiyo maana nimeamua kujiachia nao kama mashabiki wangu“.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.