Mwana FA afunguka kuhusu kumhonga mwanamke iliampende

Rapa mkali kutoka Tanzania Mwana FA ni mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri katika muziki. Ameweza kuachia nyimbo ambazo zimevuma Afrika Mashariki.

Kwa mara ya kwanza msanii huyo alifunguka kuhusu ishu ya wanaume kuwahonga wanawaka ili wawapende. Kulingana na yeye, hajawai kumhonga mwanamke yeyote katika maisha yake.

download latest music    

 

Akiongea na Risasi Vibes, Mwana FA alisema;

“Nihonge ili nipate nini, sijawahi kuhonga hata siku moja najua wengi wanaweza wasiamini lakini ndiyo hivyo, tabia hizo naishia kuziona kwa washkaji zangu huku mtaani lakini kwangu hazijawahi kuwepo maana kitendo hicho nakichukulia kama biashara ya kikahaba ambayo binafsi naichukia” alisema Mwana FA

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua