“Natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni” Elizabeth Michael ‘Lulu’ afunguka kuhusu harusi atakayofanya

Ole wao wanaume waliotaka uhusiano wa kimapenzi na Elizabeth Michael ‘Lulu’. Staa huyo wa Bongo movies atakua bibi wa mtu hivi karibuni.

Bahati, msanii wa nyimbo za injili kutoka Kenya, ni miongoni mwa wanaume wengi waliotaka kumchumbia Lulu.

download latest music    

Lulu sasa yupo tayari kufanya harusi na mpenzi wake wa muda mrefu Francis Shiza ‘Dj Majizo’- mmiliki wa Redio EFM.

Elizabeth Lulu na Francis Shiza ‘Dj Majizo’

Habari hii imetokea baadaya ya kuzuka uvumi kuwa Lulu aliachana na mpenzi wake.  Akizungumza na Mtanzania, Lulu alisema kuwa wanaotamani aachane na DJ Majizo watapigwa na duwaa atakapofanya harusi na mpenzi wake.

“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu, hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,’’ Lulu alinukuliwa na Mtanzania.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere