“Nay nataka round 3 tu za boxing kwenye stage”Muigizaji Yusuph Mlela aomba kupigana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego  alitumia ukurasa wake wa Instagram kukosoa baadhi ya  wasanii wa Bongomovie huku akiwataka wafanye kazi bora pia.

Nay alidai kuwa wasanii wa Bongomovies wanapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya kwa lengo la kutaka wafanyabiashara wanaouza filamu za nje ya nchi wafungiwe kwani hawafuati  taratibu ambazo wasanii wa bongomovie wanazifata wakati wa usambazaji wa kazi zao.

download latest music    

Muigizaji Yusuph Mlela alikerwa na maneno aliyosema Ney na kuamua kumjibu kwa hasira –alimtukana na pia kuomba apigane naye ngumi.

Yusuph Mlela na Nay wa Mitego

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano.

“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela alisema.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere