Nay wa Mitego adai Diamond Platnumz na Alikiba hawamtishi, hii ndio sababu yake

Msanii wa bongo Nay wa Mitego ni mmoja wa wasanii ambao wanafanya vyema kwenye muziki. Hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya ‘Makuzi’ ambayo anaamini kuwa itafanya vizuri.

Akizungumza hivi karibuni kwenye show ya Radio One Nay alifunguka kudai kuwa yeye hana hofu kuwa wimbo wake utafanya vizuri licha ya ishu ya Diamond Platnumz na King Kiba inayowafanya wasanii wengi kutoachilia nyimbo zao kwa sababu wanahofia hazitawafikia mashabiki wao.

download latest music    

Nay alisema;

Watu wanaogopa kutoa nyimbo kwa sababu ya vungu vungu hili, kwangu huwa naona ni vitu ambavyo huwa vinapita haraka sana na huwa siviweki katika akili, ndio maana nikiwa na kitu changu ambacho nahisi kwa wakati huo kinatikiwa kwenda bila kuangalia kuna nini kinaendelea huwa natoa.

Aliendelea kwa kusema;

Muziki wangu una nguvu kuliko vitu vingine, mashabiki wangu ambao wanaamini kwenye kile ambacho nakifanya, so kelele za watu au purukushani za huko na kule hazinizui nikiwa na kitu changu nataka kukifanya.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua