Nay wa Mitego amjibu Skyner Ally baada ya kudai ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wake

Mwanamuziki wa Tanzania Nay wa Mitego hivi karibuni aliiabishwa na muigizaji wa filamu Bongo, Skyner Ally baada ya kumchana kwa kumwambia kuwa hajakuwa akimtunza mtoto wao kama anavyostahili.

Skyner na Nay wakona mtoto wa kike pamoja lakini muigizaji huyo wa filamu amedai kuwa Nay hajakuwa akimsaidia mwanae. Hii ilikuja baada ya Nay alipoweka picha ya mtoto wao mtandaoni wa Instagram huku akimsifu kwa uzuri wake.

download latest music    

Hata hivyo Skyner hakupendelea kwani Nay hajakuwa akihusika na mambo ya mwanae kwa muda mrefu sasa. Kilicho muuma zaidi ni kwamba Nay alikuwa anawadanganya mashabiki wake kuwa anawatunza wanawe vyema ilhali alikuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wa Skyner ambaye alizaa na yeye.

Inaonekana kuwa Nay aliweza kuiona post ya Skyner na kupitia mtandao wake wa Instagram, Nay aliandika kusema…

“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huh??! Jamani inatosha basiii Povuuu. Nitapeleka Matumiziiiii???. Nawapenda sana awa Watoto Wanguu?. Wasiopeleka Matumizi ya Watoto?? #Wapo,”

Haya basi, wacha tutazame watakacho kifanya hawa wawili sasa.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua