Nay wa mitego ;-Natamani kumuona Diamond Msibani.

Msanii Nay wa Mitego ambae pia alikuwa moja ya watu waliofika katika msiba wa Ruge amefunguka na kusema kuwa amekuwa akitamani sana kumuona Diamond Platinmz katika msiba wa bwana Ruge mutahaba lakini anashangaa kwanini msanii huyo hatokei.

Akiongea na waandishi wa habari, Nay wa mitego  anasem “Duniani Tunapita tu, leo hatunaye Bosi Ruge , kiukweli natamani sana kumuona Diamond hapa msibani, muda bado lakini tusubiri labda tutamuona”

download latest music    

Diamond amekuwa moja ya wasanii walioshangaza watu wengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuna alieyetegemea kutokumuona msibani ukizingatia kuwa hata yeye alipita mikononi mwa Ruge hata kama wawili hao wanasemwa kuwa na mfarakano hapo nyuma.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.