Polisi Wang’ang’ana na Dudu Baya, Wasema Atashtakiwa.

Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kufungua  jalada la uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii dhidi ya msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya.Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema wakijiridhisha na madai hayo, hatua nyingine za kisheria zitafuata.

Hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya Dudu Baya kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutoa lugha isiyofaa kimaadili kwa Marehemu Ruge.

download latest music    

Mapema jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wanamkamata Msanii DUDU BAYA kwa kosa la kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa Marehemu
Ruge Mutahaba.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.