Qboy Msafi azidi kutamba na Kamoyo kolabo yake na Mr. Blue

Mwana mitindo mashuhuri aliyejitosa katika mziki,Qboy Msafi anazidi kuonyesha kuwa anaweza kufanikisha hata baada ya kuambiwa kuwa hawezi.

Wengi walimponda kwenye mitandao wakisema kuimba hatoweza lakini kila kuchapo Qboy anazidi kujituma na kuachia nyimbo nzuri.

Diamond Platnumz aliwahi kusema kuwa alimshauri ajitume zaidi katika fani ya nguo na mitindo badala ya kuimba.

Ukiwa makini utagundua anakua kwa kasi na katika kila kazi mpya, mashairi yanazidi kuwa mazuri na hata kuimba anaimarika na kumakinika.

Itakumbukwa Qboy Msafi alikuwa katika lebo ya mziki ya Wasafi na alitoka baada ya kufanya kosa lidogo ambalo hakukusudia lingezua uamuzi uliotolewa.

Pale WCB aliwahi kusema kuwa alikuwa kama yupo shuleni anasoma na sasa amehitimu.

“Mimi nikiwa Wasafi ni kama vile mtu akiwa chuo baadae akahitimu masomo, sasa nafanya mambo yangu tu kibao” alisema pale Radio Maisha mapema mwakani,nchini Kenya.

Baada ya kuachia ‘Karorero’ na remix yake akiwa na Naiboi ambaye ni msanii kutoka Kenya, Qboy na usimamizi wa timu yake wamepiga hatua kubwa kwa muda mfupi sana na hivi karibuni mafanikio yake yatawaacha wengi vinywa wazi.

Baada ya wimbo wake Unaanzaje, ambao ulifanya vizuri pia,Qboy Msafi sasa amemshirikisha mkali wa kutoka zamani Mr. Blue kwenye Kamoyo.

Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wazuri na wakali zaidi nchini Tanzania na hata Africa ya Mashariki.

Kamoyo ni wimbo mzuri sana na ujumbe wake unaendana na hisia na maisha ya watu wengi.

Dude limeandaliwa na Mr. T Touch pamoja na Davy Marchords.

Video ya kolabo hii ni kazi yake Lucca Swahili.

Akipiga kazi kwa kasi hii na ubora huu,basi atazidi kwenda mbali kimziki.

Mashabiki wameupokea vizuri wimbo huu.

 

About this writer:

Bakari Salim